99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri Mkuu Netanyahu asema Israel itadumisha udhibiti wa usalama huko Gaza baada ya vita kumalizika (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2024
Waziri Mkuu Netanyahu asema Israel itadumisha udhibiti wa usalama huko Gaza baada ya vita kumalizika
Helikopta ya kijeshi ya Israel ikizunguka juu ya mpaka wa ukanda wa Gaza, kwa ilivyoshuhudiwa kutoka Kusini mwa Israel, Januari 18, 2024. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua)

JERUSALEM - Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Alhamisi kuwa nchi yake itadumisha udhibiti wa usalama katika Ukanda wa Gaza baada ya kumalizika kwa vita vinavyoendelea dhidi ya Kundi la Hamas, akisema kuwa Israel itafanya "udhibiti kamili wa usalama na udhibiti wa chochote kinachoingia Gaza."

Netanyahu ameuambia mkutano na waandishi wa habari huko Tel Aviv kwamba katika muda wa siku mbili zilizopita, wanajeshi wa Israel wamewaua "makumi" ya wanamgambo katika eneo la Palestina na kuharibu vifaa vya kurusha roketi.

"Vita vinaendelea katika pande mbalimbali ... hadi tupate ushindi kamili," amesema, huku akiongeza kuwa bajeti ya wakati wa vita iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni ya shekeli 582 (kama dola bilioni 155 za Kimarekani), ambayo inajumuisha shekeli za ziada bilioni 55 za ulinzi, "inawezesha jeshi kutimiza malengo ya vita na kupata ushindi."

Amesema vita huenda vitaendelea kwa "miezi mingi."

Israel imekuwa ikiendelea na mashambulizi ya mabomu yenye athari kubwa dhidi ya Gaza bila kujali wito wa kimataifa wa kutaka kusimamisha mapigano. Mashambulizi hayo yalianzishwa Oktoba 7, 2023, kufuatia mashambulizi ya Kundi la Hamas ambayo yalisababisha vifo vya watu takriban 1,200 nchini Israel.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya yenye makao yake mjini Gaza siku ya Alhamisi, idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi hayo yanayoendelea ya Israel kwenye ukanda huo imeongezeka hadi kufikia 24,620.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha