

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu Netanyahu asema Israel itadumisha udhibiti wa usalama huko Gaza baada ya vita kumalizika (3)
![]() |
Moto ukipaa angani kutoka kwenye majengo yaliyobomolewa kwenye ukanda wa Gaza, kwa ilivyoshuhudiwa kutoka Kusini mwa Israel, Januari 18, 2024. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua) |
JERUSALEM - Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Alhamisi kuwa nchi yake itadumisha udhibiti wa usalama katika Ukanda wa Gaza baada ya kumalizika kwa vita vinavyoendelea dhidi ya Kundi la Hamas, akisema kuwa Israel itafanya "udhibiti kamili wa usalama na udhibiti wa chochote kinachoingia Gaza."
Netanyahu ameuambia mkutano na waandishi wa habari huko Tel Aviv kwamba katika muda wa siku mbili zilizopita, wanajeshi wa Israel wamewaua "makumi" ya wanamgambo katika eneo la Palestina na kuharibu vifaa vya kurusha roketi.
"Vita vinaendelea katika pande mbalimbali ... hadi tupate ushindi kamili," amesema, huku akiongeza kuwa bajeti ya wakati wa vita iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni ya shekeli 582 (kama dola bilioni 155 za Kimarekani), ambayo inajumuisha shekeli za ziada bilioni 55 za ulinzi, "inawezesha jeshi kutimiza malengo ya vita na kupata ushindi."
Amesema vita huenda vitaendelea kwa "miezi mingi."
Israel imekuwa ikiendelea na mashambulizi ya mabomu yenye athari kubwa dhidi ya Gaza bila kujali wito wa kimataifa wa kutaka kusimamisha mapigano. Mashambulizi hayo yalianzishwa Oktoba 7, 2023, kufuatia mashambulizi ya Kundi la Hamas ambayo yalisababisha vifo vya watu takriban 1,200 nchini Israel.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya yenye makao yake mjini Gaza siku ya Alhamisi, idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi hayo yanayoendelea ya Israel kwenye ukanda huo imeongezeka hadi kufikia 24,620.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma