99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary asema Hungary haitaki NATO kuwa kambi dhidi?ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 06, 2023
Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary asema Hungary haitaki NATO kuwa kambi dhidi?ya China
Hafla ya kupandishwa kwa bendera ya Hungary ya kuadhimisha miaka 175 ya mapinduzi na kupigania uhuru wa Hungary Mwaka 1848, ikifanyika kwenye uwanja wa Kossuth mbele ya jengo la Bunge huko Budapest, Hungary, Machi 15, 2023. (Picha na Attila Volgyi/ Xinhua)

BUDAPEST - Serikali ya Hungary haitaki Jumuiya ya NATO kuwa kambi ya kupambana na China, Waziri wa Mambo ya Nje Peter Szijjarto amesema Jumatano wakati wa kufungwa kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO huko Brussels.

Badala ya ushindani, ushirikiano wa kunufaishana unahitajika, amesema.

Szijjarto amesema, uhusiano kati ya NATO na China haupaswi kuelezewa kama wenye mrengo wa kijeshi.

"Hatutaki NATO kuwa kambi ya kupinga China. Hatuoni maana ya ushindani, hatuoni mantiki yake, na hatuoni ni kitu gani kizuri kinaweza kutoka kwake," amesema.

Badala ya ushindani, serikali ya Hungary ina nia ya ushirikiano wa kunufaishana, ambao amesema si tu unawezekana bali pia ni muhimu, haswa katika muktadha wa mapinduzi ya sekta ya magari.

Amekumbuka mfano wa watengenezaji wa magari wa Ulaya, ambao wamekuwa "wakitegemea kabisa betri za magari ya umeme za Korea Kusini na China".

"Wale wote wanaotaka kujitenga kwa uchumi wa China na Ulaya wana hatari ya kutoa pigo kubwa kwa uchumi wa Ulaya," amesema.

Ameonya kuwa bila ushirikiano wa China na Ulaya, hakuna sekta ya magari yanayotumia nishati mpya ya Ulaya na hakuna ulinzi wa mazingira wa Ulaya utakaofanikiwa pia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha