Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary asema Hungary haitaki NATO kuwa kambi dhidi?ya China (3)
![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary Peter Szijjarto akizungumza kwenye hafla huko Debrecen, Hungary, Septemba 5, 2022. Kampuni ya kuzalisha betri kutoka China, Contemporary Amperex Technology ilitia saini mkataba wa mali isiyohamishika na Mji wa Debrecen nchini Hungay, kuashiria uzinduzi rasmi wa kiwanda chake cha pili cha Ulaya. (Picha na Attila Volgyi/Xinhua) |
BUDAPEST - Serikali ya Hungary haitaki Jumuiya ya NATO kuwa kambi ya kupambana na China, Waziri wa Mambo ya Nje Peter Szijjarto amesema Jumatano wakati wa kufungwa kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO huko Brussels.
Badala ya ushindani, ushirikiano wa kunufaishana unahitajika, amesema.
Szijjarto amesema, uhusiano kati ya NATO na China haupaswi kuelezewa kama wenye mrengo wa kijeshi.
"Hatutaki NATO kuwa kambi ya kupinga China. Hatuoni maana ya ushindani, hatuoni mantiki yake, na hatuoni ni kitu gani kizuri kinaweza kutoka kwake," amesema.
Badala ya ushindani, serikali ya Hungary ina nia ya ushirikiano wa kunufaishana, ambao amesema si tu unawezekana bali pia ni muhimu, haswa katika muktadha wa mapinduzi ya sekta ya magari.
Amekumbuka mfano wa watengenezaji wa magari wa Ulaya, ambao wamekuwa "wakitegemea kabisa betri za magari ya umeme za Korea Kusini na China".
"Wale wote wanaotaka kujitenga kwa uchumi wa China na Ulaya wana hatari ya kutoa pigo kubwa kwa uchumi wa Ulaya," amesema.
Ameonya kuwa bila ushirikiano wa China na Ulaya, hakuna sekta ya magari yanayotumia nishati mpya ya Ulaya na hakuna ulinzi wa mazingira wa Ulaya utakaofanikiwa pia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma