China yaziunga mkono kikamilifu Uturuki na Syria katika kukabiliana na athari za matetemeko ya ardhi
BEIJING - Zheng Yuandong, Ofisa wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la China (CIDCA) amesema Jumatatu kuwa, China itaziunga mkono kikamilifu na kuzisaidia Uturuki na Syria kuondokana na athari za matetemeko makubwa ya ardhi ya hivi majuzi haraka iwezekanavyo.
Zheng amesema kuwa China imekuwa ikitoa msaada na usaidizi katika nchi hizo mbili tangu matetemeko makubwa ya ardhi yalipotokea Uturuki na Syria.
“Shehena za kwanza za vifaa vya msaada zilizofadhiliwa na Serikali ya China ziliwasili Istanbul Februari 11 na 12, zikiwa zimesheheni mablanketi na mahema ya pamba yanayohitajika haraka,” Zheng amesema.
Vifaa zaidi vilivyotolewa na China, ikiwa ni pamoja na mashine za kupima mapigo ya moyo, vifaa vya uchunguzi wa ultrasonic, magari ya usafirishaji wa vifaa vya matibabu na vitanda vya hospitali vitasafirishwa wiki hii.
Ameongeza kuwa vikosi vya uokoaji kutoka China, vikiwemo vile vilivyotumwa na Serikali ya China, vimeokoa zaidi ya watu 10 walionusurika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma