99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yaziunga mkono kikamilifu Uturuki na Syria katika kukabiliana na athari za matetemeko ya ardhi (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2023
China yaziunga mkono kikamilifu Uturuki na Syria katika kukabiliana na athari za matetemeko ya ardhi
Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2023 ikionyesha kambi ya muda ya Kikosi cha Utafutaji na Uokoaji cha China nje ya uwanja wa michezo huko Antakya katika Jimbo la Hatay, Kusini mwa Uturuki, Februari 13, 2023. (Xinhua/Shadati)

BEIJING - Zheng Yuandong, Ofisa wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la China (CIDCA) amesema Jumatatu kuwa, China itaziunga mkono kikamilifu na kuzisaidia Uturuki na Syria kuondokana na athari za matetemeko makubwa ya ardhi ya hivi majuzi haraka iwezekanavyo.

Zheng amesema kuwa China imekuwa ikitoa msaada na usaidizi katika nchi hizo mbili tangu matetemeko makubwa ya ardhi yalipotokea Uturuki na Syria.

“Shehena za kwanza za vifaa vya msaada zilizofadhiliwa na Serikali ya China ziliwasili Istanbul Februari 11 na 12, zikiwa zimesheheni mablanketi na mahema ya pamba yanayohitajika haraka,” Zheng amesema.

Vifaa zaidi vilivyotolewa na China, ikiwa ni pamoja na mashine za kupima mapigo ya moyo, vifaa vya uchunguzi wa ultrasonic, magari ya usafirishaji wa vifaa vya matibabu na vitanda vya hospitali vitasafirishwa wiki hii.

Ameongeza kuwa vikosi vya uokoaji kutoka China, vikiwemo vile vilivyotumwa na Serikali ya China, vimeokoa zaidi ya watu 10 walionusurika. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha