99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yafanya gwaride kubwa la kijeshi kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa vita vya kupambana na uvamizi wa Japan na WWII

(CRI Online) Septemba 03, 2025
China yafanya gwaride kubwa la kijeshi kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa vita vya kupambana na uvamizi wa Japan na WWII

Leo Septemba 3, saa tatu asubuhi, shughuli kubwa za kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa vita vya watu wa China vya kupambana na uvamizi vya Japan na ushindi wa vita vya dunia vya kupinga ufashisti, ikiwa ni pamoja na gwaride kubwa la kijeshi, zimefanyika katika Uwanja wa Tian’anmen mjini Beijing, China.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi Xi Jinping, ametoa hotuba muhimu na kukagua gwaride hilo lililoshirikisha vikosi mbalimbali vya jeshi.

Madhumuni ya maadhimisho hayo ni “Kukumbuka Historia, Kutoa Heshima kwa Mashujaa Waliojitoa Mhanga, Kuthamini Amani na Kujenga Upya Siku za Baadaye."

Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali 26 wamehudhuria maadhimisho hayo. Maspika wa bunge, manaibu waziri wakuu, na wawakilishi wa ngazi ya juu kutoka baadhi ya nchi, wasimamizi wa mashirika ya kimataifa na viongozi wastaafu wa nchi na serikali wamealikwa kushiriki kwenye shughuli hizo. Mbali na hawa, mabalozi na waambata wa kijeshi wa nchi mbalimbali nchini China, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini China, pamoja na marafiki wa China au wajumbe wa jamaa za wale waliofariki kutoka nchi 14 zikiwemo Russia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Canada wamealikwa kushiriki kwenye shughuli hizo.

Miaka 80 iliyopita, baada ya miaka 14 ya mapambano magumu na ya kumwaga damu, taifa la China lilipata ushindi mkubwa katika vita vya kupambana na uvamizi wa Japan, ikionesha ushindi kamili katika vita vya dunia vya kupinga ufashisti. Vita vya kupambana na uvamizi wa Japan vilianza mapema zaidi na kwa muda mrefu zaidi, vikiifanya China kuwa medani kuu ya vita vya dunia vya kupinga ufashisti katika Mashariki mwa Dunia, na kutoa mchango wa kihistoria kwa ushindi wa vita vya dunia vya kupinga ufashisti. (Picha zinatoka tovuti ya Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha