

Lugha Nyingine
Kijiji cha wachezaji cha Michezo ya Dunia ya Chengdu chafunguliwa, kukaribisha wachezaji wa kimataifa
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 04, 2025
![]() |
Wageni waheshimiwa wakizindua kifaa cha kufungua kijiji kwenye hafla ya kufunguliwa kwa kijiji cha wachezaji cha Michezo ya Dunia ya Chengdu tarehe 3, Agosti. (Wang Xi/Xinhua) |
Tarehe 3 mwezi huu, kijiji cha wachezaji cha Michezo ya Dunia ya 12 kimefunguliwa mjini Chengdu, Mkoani Sichuan, China.
Kamati ya kijiji hicho imejulisha kuwa, kijiji hicho kinagawanywa katika maeneo mawili ya A na B, na kitaendeshwa kuanzia tarehe 3 hadi 18 mwezi huu. Wakati wa michezo hiyo, kijiji hicho kitatoa huduma kwa wachezaji 7,000 hivi.
Katika kijiji hicho, kuna mikahawa kwa wachezaji na maofisa, kituo cha kujiandikisha, kituo cha huduma kwa wachezaji, chumba cha matibabu, chumba cha matibabu ya jadi ya China, jimu, na kituo cha kupima dawa za kuongeza nguvu.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma