99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Watu 6 wafariki kufuatia mafuriko ya ghafla nchini Kenya

(CRI Online) April 24, 2025

Watu sita wamefariki katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kufuatia mafuriko ya ghafla yaliyosababishwa na mvua kubwa kutokea katika maeneo mengi ya jiji hilo katika siku mbili zilizopita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi jijini Nairobi, George Sedah ameonya kuwa, idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na ukweli kwamba, huenda watu wengi wamesombwa na mafuriko hayo yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Ili kukabiliana na mafuriko hayo, mamlaka za jiji hilo zimeanza kuondoa wakazi ambao nyumba zao ziko hatarini kukumbwa na mafuriko ama maporomoko ya mawe.

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya nchini Kenya imetabiri mvua kubwa kuendelea kunyesha katika siku zijazo na kuwataka wakazi kuwa waangalifu zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha