Filamu iitwayo "Vipindi 12 vya kila siku ya Wachina" yazinduliwa kwenye Banda la China katika Maonyesho ya Osaka
Filamu iitwayo "Vipindi 12 vya kila siku ya Wachina" imezinduliwa kwenye banda la China katika Maonyesho ya Osaka. Kwa njia ya jadi ya kuhesabu muda ya China, muda wa siku moja unagawanywa katika vipindi kumi na viwili, ambavyo kwa kichina vinaitwa Shichen, na kila kipindi ni saa mbili. Hekima hiyo ya mababu wa wachina inafichua falsafa ya maisha ambayo Wachina wameiandika kwenye DNA yao.
Kati ya kuchomoza na kuzama kwa jua na mwezi, saa ishirini na nne zinajirudia. Kila moja ya mwendelezo huu himilivu wa kawaida wa kila siku hutafsiri falsafa ya maisha ya watu wa China ya kuchanganya mijongeo na kuwa tuli, kufanya mambo katika wakati mwafaka, na kufuata mazingira ya asili, na kuandika simulizi za kuvutia za maisha na furaha kwa watu wa China. Bonyeza video kuangalia jinsi wachina wanavyotumia "vipindi 12 vya kila siku".
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma