99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Majaji wanawake watekeleza majukumu yao ya kila siku mjini Beijing, China (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 11, 2025
Majaji wanawake watekeleza majukumu yao ya kila siku mjini Beijing, China
Kong Dehan (kushoto), jaji katika Mahakama ya Umma ya Eneo la Haidian la Beijing, akishughulikia kesi katika mahakama hiyo Machi 6, 2025.(Xinhua/Huang Bohan)

Jana Tarehe 10 Machi ilikuwa ni Siku ya Majaji Wanawake Duniani, ambayo iliwekwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mwaka 2021 ili kusisitiza mchango wa wanawake katika mfumo wa mahakama na kuwatia moyo wanawake zaidi kutekeleza majukumu ya kimahakama.

Kabla ya Siku hiyo, waandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua walitembelea majaji wanawake wa Mahakama ya Umma ya Eneo la Haidian la Beijing. Majaji hao wanawake wanashiriki kwa umakini katika huduma za ofisini na nje ya ofisi kama vile kufungua kesi na mambo ya mashtaka, hukumu za kesi mahakamani, kusuluhisha migogoro, kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa mahakama, na kampeni za habari za kujenga uelewa wa umma.

Kwa hekima na bidii yao, majaji hao wanawake wanaheshimu uhalali wa mahakama za kisheria, na kulinda haki na usawa kwa jamii. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha