

Lugha Nyingine
Dunia yafikia makubaliano ya msingi ya tabianchi kwenye Mkutano wa COP29 (2)
BAKU - Kifurushi cha makubaliano ya Tabianchi kimefikiwa mapema Jumapili kwenye Mkutano wa 29 wa Nchi Watia saini kwenye Mkataba wa Mfumokazi wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) mjini Baku, Azerbaijan ambapo makubaliano hayo yanajumuisha maamuzi juu ya Lengo Jipya la Pamoja la Kutathminiwa kwa ufadhili wa tabianchi na masuala yanayohusiana na utaratibu wa soko la kaboni duniani chini ya Kifungu cha 6 cha Mkataba wa Paris.
Makubaliano hayo yameweka malengo ya ufadhili wa tabianchi baada ya Mwaka 2025, yakijumuisha ufadhili wa dola angalau bilioni 300 za Kimarekani kwa mwaka kutoka nchi zilizoendelea na lengo pana la ufadhili wa tabianchi wa dola angalau trilioni 1.3 kwa mwaka ifikapo Mwaka 2035 ili kuunga mkono nchi zinazoendelea kuchukua hatua za tabianchi.
Msingi wa kujengea
"Kufikia makubaliano katika COP29 ni muhimu kwa kuendelea kudumisha kikomo cha ongezeko la joto duniani cha nyuzi joto 1.5," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameandika katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X.
Guterres ameongeza kuwa makubaliano hayo "lazima yatekelezwe kwa pande zote na kwa wakati. Natoa wito kwa serikali za nchi mbalimbali kufanya hivyo haraka."
Mipangilio hiyo inatarajiwa kuweka msingi kwa nchi zinazoendelea kuchukua hatua za tabianchi na kuwasilisha raundi mpya ya mchango iliyoamuliwa wa taifa mwaka ujao.
Pande takriban 200 zimevunja mkwamo wa miaka mingi katika majadiliano ya pande nyingi, hatimaye kuafikianakuhusu utaratibu wa soko la kimataifa la kaboni chini ya Kifungu cha 6 cha Mkataba wa Paris. Inaashiria kukamilika kwa kanuni za utekelezaji wa utaratibu wa soko chini ya Kifungu cha 6 na kutatua suala la mwisho lililokuwa limesalia ndani ya Mkataba wa Paris.
Aidha, mkutano huo pia umefikia maamuzi kuhusu masuala mbalimbali, yakiwemo ya utaratibu wa biashara ya kaboni, utekelezaji wa matokeo ya Mfumo wa Ufuatiliaji (Global Stocktake), mpango kazi wa upunguzaji wa kazi, na marekebisho ya lengo la dunia.
Katika hotuba yake wakati wa kufunga mkutano wa mashauriano, Zhao Yingmin, mkuu wa ujumbe wa China na naibu waziri wa ikolojia na mazingira wa China, alisisitiza kuwa binadamu ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na katika kukabiliana na msukosuko wa tabianchi, umoja na ushirikiano ni njia pekee zinazowezekana.
Mchango wa China
Kwenye mkutano huo wa COP29, Liu Zhenmin, mjumbe maalum wa China kuhusu mabadiliko ya tabianchi, amesema kuwa katika muongo mmoja uliopita, China imekuwa moja ya nchi zinazopunguza matumizi ya nishati kwa kasi zaidi duniani, ikiokoa tani takriban bilioni 1.4 za makaa ya mawe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma