99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yashuhudia safari za watalii milioni 765 wa ndani katika likizo ya siku 7 ya Siku ya Taifa (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2024
China yashuhudia safari za watalii milioni 765 wa ndani katika likizo ya siku 7 ya Siku ya Taifa
Watalii wakitembelea eneo la kivutio cha watalii la Mlima Mingsha na Chemchemi ya Hilali katika Mji wa Dunhuang, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China, Oktoba 4, 2024. (Picha na Zhang Xiaoliang/Xinhua)

BEIJING – Idadi ya watalii wa ndani wa China imefikia milioni 765 katika likizo ya siku 7 ya Siku ya Taifa iliyomalizika Jumatatu wiki hii, ikiwakilisha ongezeko la asilimia 5.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo, takwimu kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zimeonyesha.

Idadi hiyo ni asilimia 10.2 zaidi ya ile ya kipindi kama hicho Mwaka 2019, wizara hiyo imesema.

Thamani ya jumla ya matumizi katika manunuzi ya watalii hao wa ndani imezidi yuan bilioni 700 (dola za kimarekani kama bilioni 99.3) katika kipindi hicho, ikiongezeka kwa asilimia 6.3 kuliko mwaka jana na asilimia 7.9 ikilinganishwa na Mwaka 2019, kwa mujibu wa wizara hiyo.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha