99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yarusha kwa mafanikio kundi jipya la satalaiti kwenda anga ya juu (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2024
China yarusha kwa mafanikio kundi jipya la satalaiti kwenda anga ya juu
Roketi iliyoboreshwa ya kubeba mizigo ya Long March-6 iliyobeba kundi jipya la satalaiti ikiruka kutoka Kituo cha Kurusha Satalaiti cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China, Agosti 6, 2024. (Picha na Zheng Bin/Xinhua)

TAIYUAN - China imetuma kundi jipya la satalaiti kwenda anga ya juu siku ya Jumanne kutoka Kituo cha Kurusha Satalaiti cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa nchi hiyo ambapo satalaiti hizo 18 ni kundi la kwanza la kizazi cha kwanza cha satalaiti za Spacesail ambazo zitawapa watumiaji wa kimataifa huduma za intaneti ya kasi ya kuchakata data kubwa kwa haraka, kasi kubwa na yenye ufanisi mkubwa, Kampuni ya Great Wall ya China ambayo ni mtoaji huduma hiyo imesema.

Satalaiti hizo zilirushwa majira ya saa 8:42 Mchana (Kwa saa za Beijing) zikiwa zimepakiwa ndani ya roketi iliyoboreshwa ya kubeba mizigo ya Long March-6 na kuingia kwa mafanikio kwenye obiti yake iliyopangwa awali.

Urushaji huo unamaanisha ni safari ya 530 kwenda anga ya juu kwa roketi za kubeba mizigo za Long March.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha