99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Njia ya Kupitisha Nishati ya Mashariki ya China Yafanyiwa Ukaguzi (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2024
Njia ya Kupitisha Nishati ya Mashariki ya China Yafanyiwa Ukaguzi
Wafanyakazi wa Kampuni ya Gridi ya Taifa ya China tawi la Hefei wakifanya ukaguzi na ukarabati wa juu kwenye mnara ya namba 3418 ya laini ya umeme ya Jiansu katika Wilaya ya Lujiang, Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui, China, Aprili 9.

Kuanzia tarehe 4 hadi 15 Aprili, laini ya umeme ya ±800KV ya Jiansu ya China itakuwa ikifanyiwa kazi ya ukaguzi na ukarabati wa kila mwaka. Kupitia ukarabati huo wa pande zote, kiwango cha uhakika wa usambazaji umeme wa laini hiyo kitaboreshwa zaidi.

Laini hiyo ya umeme ya Jiansu ni moja kati ya njia kuu za mradi wa "kupitisha umeme kutoka magharibi kwenda mashariki" nchini China, ambayo ina urefu wa kilomita 2,080 na inapita mikoa na miji mitano ya Sichuan, Chongqing, Hubei, Anhui, na Jiangsu. Kila mwaka mradi huo unaweza kusafirisha nishati safi ya umeme zaidi ya bilioni 30 kilowati-saa kwa mkoa wa Jiangsu.

(Picha na Du Yu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha