99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni

(CRI Online) Februari 18, 2024
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
Wanafunzi wakitazama kazi za sanaa kwenye Maonyesho ya Ubunifu wa Dragoni huko Nairobi, Kenya Februari 15, 2024. (Picha/Xinhua)

Maonyesho ya kisanii yanayolenga kuonyesha sifa tofauti za dragoni wa China yamefanyika Alhamisi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya.

Hafla hiyo iliyofanyika kwa siku nzima, na kupewa jina la Maonyesho ya Ubunifu wa Dragoni, iliangazia kazi za sanaa zaidi ya 40 na kuandaliwa na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Ufundi ya Shandong. Walimu na wafanyakazi, wanafunzi na umma wameshiriki kwenye maonyesho ya michoro ya ukutani na picha za michoro, ambayo iliwasilisha sifa mbalimbali za dragoni wa China.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Zhou Xiaodong alisema maonyesho hayo yaliyofanyika wakati sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China inaendelea, yatasaidia kuonesha utajiri wa utamaduni wa China kwa watu wa Kenya. Amesema mwaka 2024 ni mwaka wa dragoni, au Loong kwa lugha ya Kichina, unaashiria bahati, ustawi na nguvu, akibainisha kuwa maonyesho hayo yamefanyika wakati muafaka ili kusaidia kuongeza uelewa wa tamaduni mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha