99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Vo Van Thuong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 14, 2023
Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Vo Van Thuong
Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Vo Van Thuong kwenye Ikulu ya Hanoi, Vietnam asubuhi ya tarehe 13, Desemba kwa saa za Vietnam. (Picha na Ju Peng/Xinhua)

Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Vietnam Vo Van Thuong kwenye Ikulu ya Hanoi, Vietnam asubuhi ya tarehe 13, Desemba kwa saa za Vietnam.

Kwenye mazungumzo hayo, Rais Xi Jinping amesema, kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambayo ina umuhimu wa kimkakati kunaendana na maslahi ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili. Na kwamba, pande hizo zinatakiwa kuimarisha mwongozo wa kisiasa, kuimarisha mshikamano na uratibu, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana, kuongeza mwongozo wa maoni ya umma, na kushughulikia tofauti ipasavyo.

Kwa upande wake Vo Van Thuong amesema, uhusiano wa Vietnam na China haujawahi kuwa kamilifu, wa kina na wa kirafiki kama ulivyo sasa. Amesema, kuendeleza uhusinao na China siku zote kumekuwa kipaumbele cha juu na chaguo la kimkakati la chama na serikali ya Vietnam.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha