

Lugha Nyingine
Idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza yazidi 18,000 (6)
![]() |
Mtu aliyejeruhiwa akihamishiwa hospitali katika Mji wa Deir el-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 11, 2023. (Xinhua) |
GAZA - Msemaji wa Wizara ya Afya ya Gaza Ashraf al-Qedra ametangaza kwamba idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kutokana na vita kati ya Kundi la Hamas na Israel tangu Oktoba 7 imezidi 18,000 akisema kuwa katika muda wa saa 24 zilizopita miili ya Wapalestina 208 waliokufa imehamishiwa hospitalini kwenye Ukanda wa Gaza, na Wapalestina 416 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel.
Al-Qedra amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu kwamba, hadi kufikia Jumatatu, Wapalestina jumla ya 18,205 wameuawa na wengine 49,645 kujeruhiwa katika vita hivyo.
Ametoa wito kwa timu za madaktari duniani kote kwenda katika Ukanda wa Gaza kusaidia shughuli za kuokoa maisha ya waliojeruhiwa, huku akiongeza kuwa mamia ya watu waliojeruhiwa wanasubiri kuondoka Gaza ili kupata matibabu.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma