99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi katika Mji wa Shanghai (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023
Rais Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi katika Mji wa Shanghai
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikagua eneo la makazi ya watu wanaoishi kwenye nyumba za kupanga zinazofadhiliwa na serikali mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 28, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

SHANGHAI - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amefanya ziara ya ukaguzi katika Mji wa Shanghai, Mashariki mwa China kuanzia Jumanne hadi Jumatano ambapo katika ziara yake hiyo, amekagua Soko la Mabadilishano la Shanghai Futures, maonyesho ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia ya Shanghai, na jumuiya ya makazi ya watu wanaoishi kwenye nyumba za kupanga zinazofadhiliwa na serikali.

Rais Xi amefahamishwa kuhusu juhudi za mji huo wa Shanghai katika kuimarisha ushindani wake kama kituo cha mambo ya fedha cha kimataifa, kujenga mji huo kuwa kituo cha kimataifa cha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na kujenga miradi ya nyumba za kupangisha zinazofadhiliwa na serikali.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha