99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wanasayansi wa China waanza safari ya 13 ya utafiti?wa kisayansi katika Bahari ya Aktiki (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2023
Wanasayansi wa China waanza safari ya 13 ya utafiti?wa kisayansi katika Bahari ya Aktiki
Picha hii iliyopigwa Julai 12, 2023 ikionyesha watafiti wa China wa safari ya 13 ya utafiti wa kisayansi katika Bahari ya Aktiki huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Wei Hongyi)

SHANGHAI - Wanasayansi wa China wameanza safari ya 13 ya utafiti wa kisayansi katika Bahari ya Aktiki Jumatano kwa kutumia meli ya kwanza ya China ya kupasua barafu kwenye ncha, Xuelong 2 kutokea Shanghai, Mashariki mwa China.

Safari hiyo ya kitafiti, iliyopangwa na kuratibiwa na Wizara ya Maliasili ya China inalenga kufanya uchunguzi wa jiolojia na jiofizikia ya miamba ya katikati ya bahari, pamoja na hali ya hewa ya baharini, barafu ya bahari, uchunguzi wa mazingira baharini na chini ya ardhi, na uchunguzi wa biomasi na vichafuzi vya mazingira.

Itaboresha uwezo wa China katika maeneo ya ulinzi wa mazingira ya Bahari ya Aktiki na tathmini ya uchafuzi wa bahari, na itapata taarifa na data muhimu zinazohitajika kwa ajili ya utafiti unaohusiana, kama vile mienendo ya miamba ya katikati ya bahari.

Pia timu hiyo ya watafiti itafanya kazi na wanasayansi kutoka nchi zikiwemo Russia na Thailand katika utafiti unaofaa ili kukuza ushirikiano wa kimataifa katika safari za kisayansi katika Bahari ya Aktiki.

Timu hiyo inatarajiwa kurejea Shanghai mwishoni mwa Septemba baada ya safari yenye urefu wa maili 15,500 za baharini.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha