Maktaba ya vijijini yaamsha?shauku ya watoto kupata ujuzi?katika Mkoa wa Yunnan, China (2)
Mto Nujiang, unaotiririsha maji kutoka kwenye Milima ya Tanggula kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, huchonga njia yake kupitia milima ya Yunnan ambako korongo la kuvutia unaundwa. Kwenye ncha ya kaskazini kabisa ya korongo la Mto Nujiang, ndipo kilipo Kijiji cha Qiunatong, ambacho ni nyumbani kwa maktaba ya kipekee iitwayo "Banshan Huayu". "Harufu nzuri ya vitabu inanikumbusha harufu nzuri ya maua," Gan Wenyong, mmiliki wa maktaba hiyo amesema.
Kijiji cha Qiunatong, ambacho ni sehemu ya kuzaliwa kwa Gan, kilikuwa kimeingia katika umaskini mbaya. Kwa sababu ya matatizo ya kifedha, alikosa fursa za elimu wakati wa utoto wake. Badala yake, alifanya kazi za shamba, kuchunga ng'ombe, kukusanya mimea, na kulisha nguruwe. Hata hivyo, Mwaka 2006, Gan alichukua fursa ya kujiendeleza kielimu wakati Sheria ya Elimu ya Lazima iliyorekebishwa iliondoa malipo ya ada na michango mingineyo. Akiwa na umri wa miaka 14, alianza kusoma darasa la nne, amalize masomo yake ya shule kwa michango kutoka kwa wahisani na baadaye akaandikishwa chuo kikuu.
Baada ya kumaliza mtihani wa kuingia chuo kikuu, Gan alirudi katika kijiji chake akiwa na mkusanyiko wa vitabu. Mwaka 2016, akiwa bado mwanafunzi wa chuo kikuu, Gan alirudisha kijijini Qiunatong pamoja na vitabu alivyokuwa amekusanya. Akiuza ng'ombe wawili wa familia yake ili kukusanya pesa, alibadilisha nyumba ya kulala wageni ya familia ambayo ilikuwa haitumiki na kuifanya kuwa maktaba ya "Banshan Huayu".
Gan Wenyong sasa ana maono makubwa zaidi. Anataka kuanzisha maktaba zaidi katika maeneo ya makazi ya Qiunatong. "Nataka kufanya juhudi zote kutoa mchango zaidi katika kijiji changu," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma