

Lugha Nyingine
Uturuki na Misri kufanya kazi kwa karibu katika masuala ya Syria na Libya (2)
ANKARA - Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amesema Alhamisi kuwa, Uturuki na Misri zitafanya kazi kwa karibu katika masuala ya kikanda, hasa kuhusu Libya na Syria.
"Tunataka kujaza ukurasa mpya tuliofungua na Misri kwa miradi ya pamoja na simulizi za mafanikio," Cavusoglu amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry anayetembelea mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Kuleta amani ya kudumu na utulivu nchini Syria ni muhimu kwa Uturuki na Misri, amesema Cavusoglu, na kuongeza kuwa nchi hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi kwa karibu na kubadilishana mawazo katika suala hili.
Cavusoglu amesema, mawaziri hao wawili pia wamejadili mipango ya kufanyika mkutano kati ya marais wa nchi hizo mbili na kuteua mabalozi.
"Tutawajulisha kwenye taarifa ya pamoja katika muda ujao kwa ajili ya kupandisha hadhi uhusiano hadi ngazi ya balozi, mpaka hapo tutaendelea kuchukua hatua," ameeleza.
Kwa upande wake, Shoukry amesema Misri iko tayari kuendeleza uhusiano wa pande mbili na Uturuki, kwa sababu nchi hizo mbili zimeunganishwa na "kihistoria ya zamani" na watu kutoka nchi zote mbili watafaidika kutokana na kukaribiana kiuhusiano kwa Ankara na Cairo.
Waziri huyo wa Misri pia amesema kuwa Misri na Uturuki zina maelewano ya pamoja kuhusu Libya.
"Tunakubaliana juu ya kuanzishwa kwa serikali ambayo itaakisi matakwa ya watu na kuhifadhi ukamilifu wa ardhi ya Libya," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma