99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Serikali ya Ufaransa yanusurika kwenye kura ya kutokuwa na imani, huku mswada unaopingwa wa marekebisho ya pensheni ukipitishwa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2023
Serikali ya Ufaransa yanusurika kwenye kura ya kutokuwa na imani, huku mswada unaopingwa wa marekebisho ya pensheni ukipitishwa
Wabunge wakiwa wameshikilia mabango wakati wa hotuba ya Waziri Mkuu Elisabeth Borne kwenye Bunge la Taifa huko Paris, Ufaransa, Machi 16, 2023. (Picha na Rit Heize/Xinhua)

PARIS - Hoja mbili za kutokuwa na imani dhidi ya serikali ya Ufaransa zilishindwa kuwashawishi wabunge walio wengi katika Bunge la Taifa la Ufaransa baada ya mijadala mikali iliyofuatiwa na upigaji kura ulioshindwa kufikia kura za kutosha Jumatatu alasiri.

Hii inamaanisha kuwa muswada wa serikali wa marekebisho ya pensheni ambao haukupendwa na watu wengi nchini humo unachukuliwa kuwa umepitishwa bila kupigiwa kura kwenye Baraza la Chini la Bunge la Taifa. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron sasa ana siku 15 kutunga sheria hiyo.

Hoja ya kwanza ya vyama vingi, iliyowasilishwa na kundi la upinzani la LIOT, ilipata uungaji mkono wa kura 278 miongoni mwa wajumbe wote, ikikosa kura tisa pekee kati ya 287 zinazohitajika kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Elisabeth Borne.

Hoja ya pili, iliyowasilishwa na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally, ilipata uungaji mkono wa kura 94 pekee.

Waziri Mkuu Borne siku ya Alhamisi wiki iliyopita alitumia Ibara ya 3 ya Kifungu cha 49 cha Katiba ya Ufaransa ambacho kinaruhusu serikali kulazimisha kupitishwa kwa mswada tata wa marekebisho ya pensheni bila kupigiwa kura katika Bunge la Kitaifa.

Kufuatia kitendo hiki, wabunge kupitia kambi za kisiasa walijipanga kuwasilishwa hoja za kutokuwa na imani na serikali ya Rais Macron ambazo hata hivyo zimekwama kupata uungaji mkono bungeni.

Hali ya wasiwasi imezidi kuwa mbaya katika sehemu mbalimbali nchini Ufaransa. Maandamano huko Paris na Lille yalitawanywa na polisi kwa kurusha mabomu ya kutoa machozi.

Chini ya mswada huo tata Serikali ya Ufaransa inataka kurefusha umri wa kustaafu kutoka miaka 62 ya sasa hadi 64 ifikapo Mwaka 2030, na kiwango cha chini cha pensheni cha uhakika kitaanzishwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha