

Lugha Nyingine
Mnara wa kusafirisha umeme wenye urefu sawa na jengo la ghorofa 60, wakamilika kuundwa mkoani Sichuan
Tarehe 12, Machi, Mnara wa N2017 wa mradi wa usafirishaji na ubadilishaji wa umeme 500 kV wa Yuecheng II wa Nguvu ya Umeme ya Sichuan ya Mtandao wa Umeme wa China umeundwa tayari kwenye sehemu yenye mwinuko wa mita 2,300 kutoka juu ya bahari katika Wilaya ya Zhaojue, Eneo linalojiendesha la Wayi la Liangshan la Mkoa wa Sichuan, China. Mnara huu una urefu wa mita 169 ambao ni mnara wa kusafirisha umeme wenye urefu wa juu zaidi mkoani Sichuan.
Mnara wa N2017 wenye urefu wa mita 169, urefu wake ni mara 2.4 ya urefu wa mnara wa kawaida wa usambazaji wa kV 500, ni sawa na urefu wa jengo lenye ghorofa 60.
Habari zinasema kuwa uwekezaji wa jumla wa mradi wa usambazaji na mageuzi wa umeme wa Yuecheng II wa kV 500 ni yuan bilioni 5.3, na urefu wa jumla wa njia ya usafirisha umeme ni kilomita 695. Baada ya mradi huo kuanza kutumika, utaongeza zaidi uwezo wa kusafirisha umeme wa vituo kama vile Chengdu na maeneo la kusini mwa Sichuan kwa kWh milioni 1.6.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma