Wanawake wawili wa kuendesha winchi wachangia ujenzi wa mji
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2023
![]() |
Xu Yindi akiendesha winchi kwenye chumba cha dereva chenye kimo cha makumi ya mita kutoka ardhi. (Picha/Miao Zijian) |
Katika mapali pa ujenzi wa “Sunhexiaoying” huko Hefei, Mkoa wa Anhui wa China, wafanyakazi wanawake wawili wanaendesha winchi kubwa , ambao ni Xu Yindi mwenye umri wa miaka 38 na Wu Li mwenye umri wa miaka 39.
Xu Yindi ni dereva wa winchi kutoka tawi la Shanghai la Kampuni ya Reli ya China. Anaendesha winchi kwenye chumba kidogo chenye kuta nne za vioo ambacho kimo chake kinafikia makumi ya mita kutoka ardhi.
Wu Li ni mfanyakazi anayetoa ishara kwenye ardhi kwa ajili ya uendeshaji winchi wa Xu Yindi. Chini ya ushirikiano mzuri wa watu hao wawili, vitu vya raslimali za ujenzi vinanyanyuliwa na kupelekwa tena na tena kwa usahihi kwenye nafasi zinazotakiwa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma