99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uingereza na Umoja wa Ulaya zafikia makubaliano mapya baada ya Brexit kuhusu Ireland Kaskazini (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2023
Uingereza na Umoja wa Ulaya zafikia makubaliano mapya baada ya Brexit kuhusu Ireland Kaskazini
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak (Kulia) akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen mjini Berkshire, Uingereza, Februari 27, 2023. (Simon Walker/Mtaa No. 10 wa Downing/ Xinhua)

LONDON - Uingereza na Umoja wa Ulaya (EU) Jumatatu zimekamilisha mpango mpya wa biashara baada ya Brexit kuhusu Ireland Kaskazini.

Makubaliano hayo -- yaliyopewa jina la "Mfumokazi wa Windsor" – yamepitishwa kushughulikia Itifaki ya Ireland Kaskazini, inayolenga kurahisisha masuala ya biashara yaliyojitokeza baada ya kupitishwa kwa Itifaki hiyo.

Baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa miezi kadhaa, mfumokazi huo ulitangazwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen baada ya mkutano wao huko Windsor karibu na London.

"Ninafuraha kuripoti kwamba sasa tumepata mafanikio makubwa," Sunak alisema kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na von der Leyen. "Kwa pamoja, tumebadilisha Itifaki ya awali na leo tunatangaza Mfumokazi mpya wa Windsor."

"Hii inamaanisha tumeondoa hisia zozote za mpaka katika Bahari ya Ireland," amesema.

Sunak ameuita Mfumokazi wa Windsor "hatua ya mabadiliko" kwa watu wa Ireland Kaskazini.

Kwa upande wake von der Leyen amesema Mfumokazi mpya wa Windsor uko hapa ili kuwanufaisha watu wa Ireland Kaskazini na kuunga mkono jumuiya zote zinazoadhimisha amani katika Kisiwa cha Ireland.

"Sote wawili tumejitolea kwa dhati kutafuta suluhisho la kivitendo kwa watu na kwa jamii zote za Ireland Kaskazini," mkuu huyo wa EU amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha