99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wajapan wawaaga kwa kuwapungia mkono wa kwaheri panda wengine watatu wanaorejea China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2023
Wajapan wawaaga kwa kuwapungia mkono wa kwaheri panda wengine watatu wanaorejea China
Wafanyakazi wakimhamisha panda Eimei katika eneo la Adventure World huko Shirahama, Jimbo la Wakayama, Japan, Februari 22, 2023. (Xinhua/Yue Chenxing)

SHIRAHAMA, Japan – Panda Eimei ambaye amekuwa akiishi Japan kwa miaka 28, ameondoka kwenye mbuga ya mandhari ya Wakayama iliyoko Magharibi mwa Japan pamoja na watoto wake majike mapacha kurejea China siku ya Jumatano.

Panda huyo Eimei dume mwenye umri wa miaka 30, pamoja na watoto wake majike mapacha Ouhin na Touhin wenye umri wa miaka minane waliozaliwa Japan, wameondoka kwenye makazi yao ya sasa huko Adventure World, mbuga ya mandhari katika Mji wa Shirahama, Japan.

Karibu Saa 1:15 jioni kwa saa za Japan, panda hao watatu walipanda ndege ambayo ilipaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kansai hadi kituo kilichoko Mkoa wa Sichuan nchini China, wakisindikizwa na Koji Imazu, mkurugenzi wa bustani hiyo.

Kabla ya kuondoka kwao, hafla ya kuwaaga ilifanyika katika bustani hiyo Jumanne alasiri, watalii wapatao 2,000 walishiriki kwenye hafla hiyo, ambayo ilitangazwa moja kwa moja kwenye Mtandao wa YouTube na kutazamwa na watazamaji 13,000.

"Familia ya Eimei imeanzisha urafiki wa pande zote na watu wa Japan kwa michango isiyoweza kubadilishwa na maalum katika kukuza urafiki wa watu wa China na Japan," Konsela Mkuu wa Ubalozi wa China huko Osaka Fang Wei amesema kwenye hafla hiyo.

Siku ya Jumanne, panda maarufu jike Xiang Xiang aliyezaliwa Japan aliondoka kwenye Bustani ya Wanyama ya Ueno ya Tokyo na kufika katika kituo kikubwa cha utafiti na uzalianaji wa panda katika Mji wa Ya'an, Mkoa wa Sichuan nchini China.

Siku hiyo ya Jumanne pia ilikuwa ya kuadhimisha kuonekana kwa panda hao watatu kwa mara ya mwisho nchini Japan, wakati mashabiki wengi waliposubiri kwa saa nyingi katika foleni kwenye bustani hiyo, wengine wakitokwa machozi, kuaga kwa kupiga picha za Eimei na Touhin wakati wakitafuna mianzi.

Dada pacha wa Touhin, Ouhin, hakuonekana kwa umma kwa kuwa alikuwa akionyesha dalili za kuwa kwenye siku zake.

"Nimenasa picha za Eimei akifurahia chakula huku akiwa amefumba macho!" Aya Ito msanifu wa maumbo ya ndani ya nyumba amesema kwa furaha tele huku akitoka nje ya nyumba ya panda.

Eimei, au Yong Ming kwa Lugha ya Kichina, ambaye umri wake ni sawa na binadamu wa miaka 90, ndiye panda mkubwa zaidi aliyewahi kuishi Japan. Mwaka jana, Eimei aliteuliwa kama balozi maalum wa urafiki wa China na Japan. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha