

Lugha Nyingine
Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China Wang Yi asema Uhusiano wa Wenzi kati ya China na Russia haulengi upande wa tatu (2)
![]() |
Rais wa Russia Vladimir Putin akikutana na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, huko Moscow, Russia, Februari 22, 2023. (Xinhua/Cao Yang) |
MOSCOW – Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China Wang Yi Jumatano alipokutana na Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia katika zama mpya siku zote haulengi upande wa tatu, wala hauvumilii kuingiliwa au kushurutishwa na upande wa tatu.
Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC amesema kwamba uhusiano kati ya China na Russia umejengwa kwenye msingi imara wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, pamoja na utulivu na uthabiti kutokana na kupitia uzoefu wa zamani.
Amesema, muhimu zaidi, hii ni kwa sababu Dunia yenye ncha nyingi na demokrasia kubwa zaidi katika uhusiano wa kimataifa, ambayo China na Russia kwa pamoja zinaunga mkono, inaendana na mkondo wa nyakati na matarajio ya nchi nyingi.
Wang amewasilisha kwa Putin salamu za upendo kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping. Ameeleza kuwa marais hao wawili walifanya mkutano muhimu kwa njia ya video mwishoni mwa mwaka jana, ambao umejenga mwelekeo wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika mwaka mpya.
Amesema hali ya sasa ya kimataifa ni ngumu na ya kusikitisha, lakini uhusiano kati ya China na Russia ambao umestahimili mabadiliko makubwa ya hali ya Dunia, umekomaa, ni mgumu na thabiti kama mlima Tai.
“Ingawa migogoro na machafuko mara nyingi huibuka, changamoto na fursa zipo kwa wakati mmoja,” Wang amesema, huku akiongeza kuwa huu ni upembuzi yakinifu wa historia.
Kwa upande wake Rais Putin amemwomba Wang kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi, Putin amesema, Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefungua matarajio mapya kwa maendeleo ya China.
Putin amesema hivi sasa uhusiano kati ya Russia na China unaelekea kwenye malengo yaliyowekwa, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali na uratibu katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, BRICS na mashirika mengine ya pande nyingi unazaa matunda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma