99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Askari wa zima moto wanapambana na moto mkubwa huko Florida, Marekani (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2023
Askari wa zima moto wanapambana na moto mkubwa huko Florida, Marekani
Picha hii ya iliyopigwa kwenye skrini ya video iliyotolewa na Idara ya Uokoaji kwenye Moto ya Kaunti ya Osceola na EMS ikionyesha askari wa zima-moto wakifanya kazi ya kuzima moto mkubwa huko Kissimmee, Florida, Marekani, Februari 16, 2023. (Uokoaji wa Moto wa Kaunti ya Osceola na EMS/Kutumwa kupitia Xinhua)

WASHINGTON - Askari wa zima moto wanajitahidi kudhibiti moto mkubwa huko Kissimmee, Kusini-Mashariki mwa Jimbo la Florida nchini Marekani, uliozuka siku ya Alhamisi.

Moto huo umezuka kwenye shamba la miche asubuhi ya Alhamisi, ukihusisha pia eneo lenye ukubwa wa ekari mbili lenye kuhifadhi vyungu vya plastiki vya kuwekea maua, kwa mujibu wa mamlaka ya dharura.

Vyungu hivyo vya plastiki kwenye duka la rejareja karibu na shamba hilo la miche ziko eneo la wazi, na wazima moto wanajaribu kulinda jengo la duka hilo kubwa dhidi ya moto.

Idara ya Uokoaji na Zimamoto ya Kaunti ya Osceola na EMS imesema Alhamisi adhuhuri kwamba "askari wa zima moto 75 na magari 21 wanaendelea na kazi ya kudhibiti moto huo kabisa, huku ukitarajiwa kuzimwa kabisa ndani ya saa moja au zaidi."

"Tunakadiria itachukua saa nyingine za ziada kwani kuna kiwango kikubwa cha plastiki zilizoyeyuka, n.k.," idara hiyo imesema.

Kanda za video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miale ya moto na moshi mnene na mweusi ukipanda angani.

Wataalam wa zima moto wamefunga vifaa vya ufuatiliaji wa hewa na wako tayari kutekeleza amri za uhamishaji watu, ikiwa italazimu, maofisa wamesema.

Hakuna majeruhi wameripotiwa hadi kufikia sasa.

Shamba hilo la miche liko kwenye umbali wa kilomita 21 kutoka Walt Disney World, eneo la mapumziko la burudani karibu na miji ya Orlando na Kissimmee. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha