99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Msaada mpya wa kibinadamu wa China wawasilishwa Syria iliyokumbwa na tetemeko la ardhi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2023
Msaada mpya wa kibinadamu wa China wawasilishwa Syria iliyokumbwa na tetemeko la ardhi
Shehena ya msaada wa kibinadamu kutoka China ikihamishwa kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus huko Damascus, Mji Mkuu wa Syria, Februari 15, 2023. (Picha na Ammar Safarjalani/Xinhua)

DAMASCUS - Ndege ikiwa na shehena za msaada wa kibinadamu kutoka China imetua Damascus siku ya Jumatano ili kusaidia Syria kuondokana na athari za matetemeko ya ardhi yenye nguvu yaliyoikumba nchi hiyo wiki iliyopita.

Balozi wa China nchini Syria Shi Hongwei na Moataz Dawji, Waziri Msaidizi wa Wizara ya Tawala za Mitaa na Mazingira ya Syria, walikuwa kwenye uwanja wa ndege kushuhudia opokeaji na uhamishaji wa shehena hizo za msaada.

Akiwa kwenye uwanja huo wa ndege, Shi amewaambia waandishi wa habari kwamba msaada huo unajumuisha tani 80 za vifaa tiba, kama vile vifaa vya kusaidia upumuaji na vifaa vya kuzalisha oksijeni, pamoja na mahema, vifaa vya huduma ya kwanza, blanketi, nguo za kujikinga dhidi ya baridi, na vyakula.

Shi amesema kwamba ingawa zimetenganishwa na maelfu ya maili, China na Syria zimekuwa marafiki wazuri na wa kweli ambao husaidiana na kujaliana.

"Serikali ya China itatoa msaada zaidi wa dharura wa kibinadamu, iwe chakula au vifaa vya dawa, pamoja na vifaa vya mawasiliano ili kuunga mkono juhudi za Syria katika kukabiliana na janga la tetemeko la ardhi," balozi huyo ameongeza.

Kwa upande wake, Dawji amesema kwamba kipaumbele cha Serikali ya Syria kwa sasa ni kuwasaidia watu walionusurika na kuwapa msaada wanaohitaji, akielezea imani yake kwamba Wasyria wataweza kushinda taabu zilizotokana na maafa na kujenga upya maskani yao kwa msaada kutoka kwa marafiki kama China.

Baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyoikumba Uturuki na nchi jirani ya Syria mnamo Februari 6, China imekuwa ikitoa msaada kwa nchi hizo mbili. Chama cha Msalaba Mwekundu cha China kiliguswa mara moja, na kutoa shehena mbili za msaada wa kibinadamu kwa Syria, ambazo ziliwasili Damascus Februari 9 na 13.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha