Ofisa wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China akutana na Mabalozi wa Uturuki na Syria na kuwaelezea hatua za msaada wa dharura (2)
![]() |
Naibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China Deng Qingbo (kulia) na balozi wa Syria nchini China Muhammad Hassanein Khalil Khaddam wakishikana mikono. Picha inatoka tovuti ya Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China. |
Tarehe 7 na 8, Februari, Naibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendenleo ya Kimataifa la China Deng Qingbo alikutana na balozi wa Uturuki nchini China Abdulkadir Emin Onen na balozi wa Syria nchini China Muhammad Hassanein Khalil Khaddam, ili kuwaelezea hatua za China za kutoa msaada wa kibinadamu wa dharura kwa nchi hizo mbili.
Deng amesema, China itatoa msaada wa dharura wenye thamani ya Yuan milioni 40 (takribani Dola za Marekani milioni 5.892) kwa Uturuki, ambao utahusisha kupeleka vikosi vya uokoaji wa miji vyenye vifaa vizito na kikosi cha madaktari, na kutoa mahitaji yanayohitajika kwa dharura kwa upande wa Uturuki; itatoa msaada wa kibinadamu wa dharura wenye thamani ya Yuan milioni 30 (takribani Dola za Marekani milioni 4.418) kwa Syria, ambao utahusisha msaada wa fedha wa Dola za Marekani milioni 2 na mahitaji nyingine yanayohitajika kwa dharura kwa upande wa Syria, na pia kuharakisha kutekelezwa kwa mradi unaondelea wa msaada wa chakula. Katika mradi huo wa chakula, ngano tani 220 ziko njiani kuelekea Syria, na mchele na ngano nyingine zaidi ya tani 3,000 zitasafirishwa kwa makundi mawili hivi kariburi.
Deng amesema, Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China litashirikiana barabara na idara husika za nchi hizo mbili, ili kuhakikisha msaada huo unafika na kuwasaidia watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi kwa haraka iwezekanavyo. China itaendelea kutoa msaada kwa Uturuki na Syria kutokana na hali ya maafa na mahitaji yao halisi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma