99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi Uturuki na Syria yafikia zaidi ya 12,000 na uokoaji waingia siku ya tatu (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 09, 2023
Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi Uturuki na Syria yafikia zaidi ya 12,000 na uokoaji waingia siku ya tatu
Waokoaji wakitafuta watu walionusurika kwenye vifusi vya jengo lililobomolewa katika wilaya iliyokumbwa na tetemeko la ardhi ya Elbistan, Jimbo la Kahramanmaras, Uturuki, Februari 7, 2023. (Xinhua/Shadati)

ANKARA/DAMASCUS, - Idadi ya watu waliofariki kutokana na matetemeko mabaya ya ardhi ya Jumatatu yaliyokumba Uturuki na Syria imezidi watu 12,000, huku uwezekano wa kupata watu walionusurika ukipungua zaidi katika hali ya hewa ya baridi kabla ya saa 72 za dhahabu kuisha.

Waokoaji na watu wa kujitolea wanafanya kazi usiku kucha kutafuta walionaswa chini ya vifusi huku kiwango cha binadamu kuweza kuishi bila kula chakula au kunywa maji kikishuka sana baada ya saa 72, ambazo zinakaribia kwa kasi. Wataalamu wameonya kuwa muda wa saa 72 wa kuwaokoa walionaswa kwenye maeneo ya matetemeko ya ardhi unaweza kuwa mdogo zaidi kuliko ilivyotarajiwa, ikizingatiwa uwepo wa halijoto ya chini katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hali ambayo inaongeza hatari ya hypothermia.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde, matetemeko hayo mabaya ya ardhi ya Jumatatu katika maeneo ya Kusini mwa Uturuki na Kaskazini mwa Syria yamesababisha vifo vya watu 9,057 nchini Uturuki na 3,480 nchini Syria.

Utafutaji unaendelea

Vikosi vya utafutaji na uokoaji kutoka zaidi ya nchi 65 vimewasili katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki kutoa msaada katika juhudi za kukabiliana na tetemeko hilo, kwa mujibu wa taarifa rasmi.

Ndege iliyokuwa imebeba kikosi cha waokoaji 83 kutoka China na tani 20 za zana na vifaa vya kusaidia kwenye maafa iliwasili katika Mji wa Adana, Kusini mwa Uturuki mapema Jumatano. Mbali na zana na vifaa vya utafutaji na uokoaji, mawasiliano na matibabu, pia kikosi hicho kimekwenda na mbwa wanne wa uokoaji.

Misaada yaendelea kuingia

Wakati shughuli za uokoaji zikiendelea nchini Uturuki na Syria, nchi nyingi zimejitolea kutoa msaada.

Nchi mbalimbali duniani zikiwemo China, Lebanon, Tunisia, Jordan, Israel, Saudi Arabia na nyingine nyingi zimeendelea kutoa misaada muhimu inayohitajika sana kwa waathirika wa tetemeko hilo.

Taratibu za uokoaji na utoaji misaada zarejea kawaida nchini Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikiri siku ya Jumatano kwamba kulikuwa na matatizo katika siku ya kwanza ya kukabiliana na tetemeko la ardhi lakini hali imeimarika sasa.

Ameongeza kuwa, waathiriwa wa tetemeko la ardhi wanaweza kukaa kwa muda katika hoteli zilizoko kwenye eneo la kitalii la Mediterania lililoko Mji wa Antalya katika jimbo la a kusini la Mersin.

Rais wa Uturuki ametangaza kwamba kila familia iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi itapokea lira 10,000 za Kituruki (kama dola 531 za Kimarekani), na nyumba mpya zitajengwa katika maeneo 10 yaliyoathiriwa na tetemeko hilo la ardhi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha