

Lugha Nyingine
Huawei yafungua duka kubwa la pili nchini Saudi Arabia
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 01, 2023
![]() |
Picha iliyopigwa Januari 31, 2023 ikionyesha mteja akijaribu kompyuta janja mpakato kwenye duka jipya la Huawei huko Jeddah, Saudi Arabia. (Wang Haizhou/Xinhua) |
JEDDAH, Saudi Arabia - Kampuni kubwa ya kiteknolojia ya China Huawei Jumanne ilifungua duka kubwa jipya huko Jeddah, mji wa bandari kwenye Bahari Nyekundu nchini Saudi Arabia.
Hili ni duka la pili kufunguliwa na Huawei katika nchi hiyo ya kifalme.
Eric Yang, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji wa Kiteknolojia ya Huawei, Tawi la Saudi Arabia, amesema duka hilo jipya huko Jeddah linaonyesha nia ya Huawei kupanua biashara yake katika nchi hiyo ya kifalme na vile vile kuweka kipaumbele zaidi kwenye soko hili la kimkakati.
Duka la kwanza la Huawei nchini Saudi Arabia lilifunguliwa rasmi Februari 2, 2022 huko Riyadh, mji mkuu wa ufalme huo. Pia ni duka kubwa zaidi la Huawei nje ya China.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma