

Lugha Nyingine
Idadi ya watu waliofariki katika shambulizi la mlipuko Kaskazini Magharibi mwa Pakistan yafikia 100 (3)
![]() |
Waokoaji wakifanya kazi ya uokozi huko Peshawar, Pakistan Tarehe 31, Januari. (Xinhua/ Saeed Ahmad) |
Hospitali ya Pakistan tarehe 31, Januari ilithibitisha kuwa, katika tukio la shambulizi la mlipuko kwenye msikiti huko Peshawar, mji mkuu wa Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Kusini Magharibi mwa Pakistan, idadi ya watu waliouawa imeongezeka hadi 100 na wengine 200 wamejeruhiwa.
Ofisa wa polisi wa Peshawar Muhammad Ijaz Khan amewaambia wandishi wa habari kuwa, uchunguzi wa hatua ya kwanza umeonesha tukio hilo ni shambulizi la mlipuko wa kujitoa mhanga. Katika wakati wa mlipuko huo, kulikuwa na zaidi ya watu 350 kwenye msitiki. Waokoaji waligundua miili zaidi ya watu waliofariki chini ya vifusi vya msikiti tarehe 31. Hivi sasa uokoaji bado unaendelea.
Habari kutoka vyombo vya habari vya Pakistan zinasema, Kundi la Taliban la Pakistan lilitangaza kuhusika na shambulizi hilo, lakini baadaye likakanusha tangazo lake hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma