99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wananchi wa Tunisia waanza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2023
Wananchi wa Tunisia waanza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge
Mtu akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura mjini Tunis, Tunisia, Januari 29, 2023. Watunisia siku ya Jumapili iliyopita walianza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge, Tume Huru ya Juu ya Uchaguzi ya Tunisia (ISIE) imesema. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)

TUNIS - Wananchi wa Tunisia Jumapili walianza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge, Tume Huru ya Juu ya Uchaguzi ya Tunisia (ISIE) imesema.

Jumla ya maeneo 4,222 na vituo 10,012 vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wapiga kura saa 2 Asubuhi kwa saa za Tunisia (0700 GMT) huku kukiwa na ulinzi mkali, na upigaji kura ulikuwa umepangwa kuendelea hadi saa 12 jioni kwa saa za huko (1700 GMT).

"Idadi ya jumla ya wagombea walioshiriki duru hii ilifikia 262, wakiwemo wanawake 34," amesema Mkuu wa ISIE Farouk Bouasker katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Tunis Jumamosi usiku.

Kwa mujibu wa Bouasker, tangazo la matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi litatolewa baada ya Februari 1, na matokeo ya mwisho, baada ya kumalizika kwa rufaa, yatatangazwa kabla ya Machi 4.

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge wa Tunisia, ambao ulifanyika Desemba 17 mwaka jana, ulishuhudia idadi ndogo inayofikia asilimia 11.22 pekee ya wapigakura halali waliojitokeza kupiga kura, huku wagombea 23 pekee wakishinda na kuthibitishwa kuwa wabunge katika bunge jipya.

Rais wa Tunisia Kais Saied alitangaza Machi 30 mwaka jana kulivunja Baraza la Wawakilishi wa Wananchi, au Bunge la Taifa la Tunisia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha