

Lugha Nyingine
Blinken azuru Israel, ahimiza utulivu wa Israel na Palestina huku ghasia zikipamba moto (2)
JERUSALEM - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameitembelea Israel siku ya Jumatatu, akiwataka Waisraeli na Wapalestina kutuliza mivutano na kusisitiza ahadi ya Washington "yenye uimara wa chuma" kwa usalama wa Israeli.
Ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya nchi tatu Mashariki ya Kati, Blinken aliwasili Israel baada ya kuzuru Misri. Huu ulikuwa mkutano wake wa kwanza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu tangu Netanyahu arejee tena kwenye nafasi ya waziri mkuu Desemba 2022 akiwa kiongozi wa serikali mpya ya mrengo wa kulia uliokithiri na ya kidini.
Kwenye uwanja wa ndege alipowasili, Blinken alilaani mashambulio mabaya ya hivi majuzi kati ya Waisraeli na Wapalestina.
"Kupoteza maisha ya watu wasio na hatia katika kitendo cha ugaidi siku zote ni uhalifu mbaya," amesema, na kuongeza kuwa wito wa Israeli wa kulipiza kisasi "dhidi ya waathirika wasio na hatia siyo jibu," kwani "vitendo vya kulipiza kisasi dhidi ya raia kamwe havina uhalali."
Katika taarifa za baadaye za pamoja na Netanyahu baada ya mkutano wao, Blinken amezitaka "pande zote kuchukua hatua za haraka kurejesha utulivu na kupunguza hali hiyo."
"Tunataka kuhakikisha kuwa kuna mazingira ambayo tunaweza, natumai, wakati fulani, kuweka mazingira ambayo tunaweza kuanza kurejesha hali sawa ya usalama kwa Waisraeli na Wapalestina, ambayo bila shaka inakosekana," amesema Blinken.
Blinken amesisitiza tena ahadi ya Marekani ya suluhisho la kuundwa mataifa mawili ili kumaliza mgogoro wa Israel na Palestina.
Ziara hiyo ya Blinken imeenda sambamba na kuzuka kwa ghasia kati ya Waisraeli na Wapalestina. Tokea mwanzoni mwa Mwaka 2023, Wapalestina wasiopungua 35 wameuawa na vikosi vya Israeli, kwa mujibu wa takwimu rasmi za Wapalestina.
Netanyahu hakutaja mvutano wa kikanda katika taarifa yake. Badala yake, alizungumzia "uchokozi" wa Irani na nia yake ya kupanua kile kinachoitwa Makubaliano ya Abraham yaliyotiwa saini Mwaka 2020 ambapo Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Morocco zilikubali kurejesha kawaida uhusiano na Israeli.
Mwanadiplomasia mkuu huyo wa Marekani, amepanga pia kufanya ziara kwenye Mamlaka ya Palestina, ambapo atakutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas leo Jumanne
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma