

Lugha Nyingine
Nchi wanachama wa WTO zakabiliana na matumizi mabaya ya Marekani ya “umaalum wa kiusalama” kwa madhumuni ya kujilinda kibiashara (2)
![]() |
Picha iliyopigwa Machi 8, 2018 ikionyesha mandhari ya nje ya Ikulu ya Marekani huko Washington D.C., Marekani. (Xinhua/Ting Shen) |
GENEVA – Nchi wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) zimeishutumu Marekani kwa matumizi mabaya ya rufaa dhidi ya maamuzi ya jopo la shirika hilo la kimataifa kuhusu ushuru wa forodha na uwekaji usiofuata utaratibu wa lebo zinazoonesha asili ya bidhaa, na zimeitaka nchi hiyo kutimiza wajibu wake wa kuwa mwanachama wa WTO na kuacha mwenendo wa kuchukua hatua zake za upande mmoja na za kujilinda kibiashara.
Katika mkutano wa Bodi ya Usuluhishi wa Migogoro (DSB) uliofanyika Ijumaa, wanachama watano wa WTO -- China, Norway, Uswisi, Uturuki, na Hong Kong -- waliutaka mkutano huo wa mashauriano kupitisha maamuzi matano ya jopo kuhusu ushuru uliowekwa na Marekani kwenye chuma na aluminiamu zinazoingia nchini humo na Marekani kuweka matakwa ya kuziwekea lebo ya asili ya bidhaa zinazozalishwa Hong Kong.
Kabla ya mkutano huo, Marekani ilikuwa imekata rufaa kuhusu maamuzi manne ya jopo hilo juu ya ushuru uliowekwa na Washington kwenye uagizaji wa bidhaa za chuma na alumini kutoka China, Norway, Uswizi na Uturuki.
Marekani pia imewasilisha rufaa tofauti dhidi ya uamuzi mwingine uliotolewa mwezi uliopita, ambapo Washington iliziwekea lebo kwa makusudi bila kufuata kanuni bidhaa zilizozalishwa Hong Kong kwa kuzitambua kama "zilizotengenezwa China." Mabadiliko hayo ya asili ya bidhaa hizo zilizongizwa Marekani yaliamuliwa kuwa yasiyo "na sababu" na jopo la DSB.
Nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi duniani pia ilitangaza kuwa itaahirisha utekelezaji wa ripoti ya jopo hilo kuhusiana na malalamiko yaliyofunguliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwenye chombo hicho yanayoilalamikia Marekani kutoza ushuru wa kuuza bidhaa chini ya bei na ushuru wa kufidia ruzuku kwenye mizeituni iliyoiva kutoka Hispania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma