

Lugha Nyingine
Thailand yakaribisha watalii wa China baada ya China kuboresha hatua za kudhibiti UVIKO-19 (5)
![]() |
Abiria wa China wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Suvarnabhumi mjini Samut Prakan, Thailand, Januari 9, 2022. (Xinhua/Rachen Sageamsak) |
BANGKOK - Thailand siku ya Jumatatu iliwakaribisha maelfu ya watalii wa China waliowasili katika mji mkuu wake wa Bangkok, ikiwa ni kundi la kwanza la watalii kufuatia China kuboresha hatua zake za kudhibiti UVIKO-19 ambapo zilianza kutekelezwa Januari 8.
Katika uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi, Naibu Waziri Mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Afya ya Umma Anutin Charnvirakul na maafisa wengine wakuu waliwakaribisha watalii 269 kutoka mji wa Xiamen wa China, ambao walilakiwa kwa maua na mifuko yenye zawadi.
“Kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaoingia Thailand kutoka China na nchi nyingine ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii ya Thailand, kuleta mapato na kuongeza nafasi za ajira kwa wananchi, jambo ambalo linachangia kuimarika kwa uchumi wa nchi hiyo,” Anutin amesema.
Amesema kuwa kwa jumla kulikuwa na usafiri wa ndege wa mara 15 kutoka China siku ya Jumatatu iliyopita, ambapo takriban abiria 3,465 wamwasili Bangkok.
Serikali ya Thailand inatarajia kupokea watalii wapatao 300,000 wa China kuzuru Thailand katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.
Anutin amesema pia siku hiyo ya Jumatatu kuwa wageni hawatahitajika kuonyesha ushahidi wa kuchanjwa chanjo, lakini wasafiri kutoka nchi zinazohitaji upimaji wa RT-PCR wanaporudi watahitajika kuwa na bima ya afya, ikiwa ni pamoja na a UVIKO-19, kabla ya kuingia Thailand.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma