99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Bunge la Marekani lililogawanyika lakutana kwa kashfa, huku Mbunge McCarthy akipoteza uchaguzi wa awali wa spika wa bunge (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2023
Bunge la Marekani lililogawanyika lakutana kwa kashfa, huku Mbunge McCarthy akipoteza uchaguzi wa awali wa spika wa bunge
Picha iliyopigwa Januari 3, 2023 ikionyesha Jengo la Bunge la Marekani, Capitol huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Bunge jipya la Marekani lililogawanyika lilikutana Jumanne adhuhuri huku kukiwa na mzozo mkali wa uongozi wa Baraza la Chini la Bunge (House of Representatives) na kashfa inayotikisa ya mbunge mteule kudanganya kuhusu wasifu wake.

Kikao hicho cha bunge kinafanyika miezi miwili baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Mwaka 2022, ambapo Chama cha Republican kilifanikiwa kushika uongozi wa Baraza la Chini la Bunge la Marekani kwa kukishinda Chama cha Democrat ambacho kimeendelea kuwa na viti vingi kwenye Baraza la Juu la Bunge la Marekani, Seneti.

Mbunge wa Bunge la Marekani Kevin McCarthy, wa Chama cha Republican anayewakilisha Jimbo la California, alipoteza katika uchaguzi wa awali wa nafasi ya Spika wa Bunge siku ya Jumanne alasiri baada ya Wabunge wa Republican 19 kuwapigia kura wengine, na kuufanya uchaguzi huo kwenda kwenye duru ya pili.

Wabunge wote wa Chama cha Democrat walimpigia kura Mbunge Hakeem Jeffries kutoka New York kuongoza kambi ya wabunge wachache bungeni wa Chama cha Democrat, na hivyo kumfanya kuwa mbunge wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Afrika katika historia kuongoza chama katika ama Baraza la Chini au Baraza la Juu, yaani Seneti.

Ikiwa hakuna mgombeaji atashinda kwa kura nyingi katika duru inayofuata, wajumbe wa Bunge watapiga kura hadi spika atakapochaguliwa.

Mbunge mteule wa Marekani George Santos, mwenye umri wa miaka 34 wa chama cha Republican kutoka New York, ni miongoni mwa wanaosubiri kuapishwa baada ya uchaguzi wa spika.

Santos hivi majuzi amekiri kudanganya kuhusu wasifu wake wa elimu na wasifu wake wa kitaaluma lakini amekataa wito wa pande mbili za vyama kumtaka asichukue wadhifa huo.

"Dhambi zangu hapa zinapamba wasifu wangu. Samahani," Santos alikiri wiki iliyopita huku akidai kuwa mabishano hayo hayatamzuia "kupata mafanikio mazuri ya kibunge."

Bunge hilo lililogawanyika huku wanachama wa Republican wakidhibiti Baraza la Chini huenda litazuia ajenda ya kupitishwa kwa miswada mbalimbali ya Rais wa Marekani Joe Biden katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Kwa kuongezea, Wabunge wa Republican wameapa kuanzisha uchunguzi mfululizo juu ya utawala wa Chama cha Democrat, wakiwa tayari kuongeza mgawanyiko zaidi juu ya vurugu za Januari 6 kwenye Jengo la Bunge, Capitol Hill.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha