99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Makamu wa Rais wa China ashiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Brazil Lula da Silva (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2023
Makamu wa Rais wa China ashiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Brazil Lula da Silva
Mwakilishi Maalum wa Rais wa China Xi Jinping, Makamu wa Rais wa China, Wang Qishan alipokutana na Rais mpya wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva mjini Brasilia, Brazil, Januari 2, 2023 alimkabidhi barua iliyotiwa saini na Rais Xi. Kwa mwaliko wa serikali ya Brazili, Wang Qishan ameshiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Luiz Inacio Lula da Silva na kukutana naye huko Brasilia. (Xinhua/Liu Bin)

BRASILIA - Kwa mwaliko wa Serikali ya Brazil, Mwakilishi Maalum wa Rais Xi Jinping wa China, Makamu wa Rais wa China Wang Qishan ameshiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na kukutana naye mjini Brasilia, mji mkuu wa Brazil.

Wakati wa kuwepo kwake nchini Brazil kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu, Wang pia alikutana na Makamu wa Rais mteule wa Brazil Geraldo Alckmin na Makamu wa Rais aliyemaliza muda wake madarakani Hamilton Mourao.

Kwenye mkutano wake na Lula, Wang alikabidhi barua iliyotiwa saini na Rais Xi na kuwasilisha salamu za pongezi na heri za Rais Xi kwa Lula pamoja na mwaliko wake kwa Lula kutembelea China.

Rais Lula ni rafiki wa watu wa China tangu zamani, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijali na kuunga mkono maendeleo ya uhusiano wa China na Brazil, Wang amesema.

Huku akieleza kwamba hivi karibuni China na Brazil zimekamilisha ajenda kuu za kisiasa za ndani, Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika kwa mafanikio, na kuchagua uongozi mpya mkuu na Komredi Xi Jinping akiwa msingi wake, na kuandaa dira ya kimkakati ya mipango ya maendeleo ya shughuli mbalimbali za Chama na Nchi ya China katika kipindi kijacho, akiongeza kuwa Brazil pia imechagua serikali mpya.

Wang ametoa mapendekezo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya China na Brazil ikiwa ni pamoja na kuhimiza mabadilishano na mawasiliano ya ngazi ya juu, kuongeza uratibu wa uhusiano wa pande nyingi, kupanua ushirikiano wa kivitendo katika uchumi na biashara na kuimarisha ushirikiano wa jumla kati ya China na Amerika ya Kusini.

Kwa upande wake, Rais Lula amemwomba Wang kuwasilisha shukrani zake za dhati na salamu za dhati kwa Rais Xi, na kumkaribisha kwa furaha Wang kushiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwake.

Amesema Brazil na China, zikiwa nchi mbili zenye ushawishi mkubwa, zinapaswa kubeba jukumu kubwa katika kukuza maendeleo ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na anatarajia kuongoza ujumbe wa kufanya ziara nchini China ili kuzidisha ushirikiano wa kivitendo wa pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, kuongeza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, na kuinua uhusiano wa Brazil na China kwenye kiwango kipya.

Katika mkutano wake na Alckmin, Wang alimpongeza kwa kuchaguliwa kwake, na kusema kuwa China na Brazil ndizo nchi kubwa zaidi zinazoendelea katika Ukanda wa Mashariki na Magharibi.

Kwa muda mrefu, ushirikiano wa kivitendo daima umefanya kazi kama "kiimarishaji" na "kiongezi" katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Wang ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha