99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Nchi 5 wajumbe wapya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zaanza kubeba wajibu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2023
Nchi 5 wajumbe wapya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zaanza kubeba wajibu
Mwakilishi wa kudumu wa Kazakhstan katika Umoja wa Mataifa Akan Rakhmetullin akiongoza hafla ya uwekaji bendera kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 3, 2023. Nchi tano -- Ecuador, Japan, Malta, Msumbiji na Uswisi -- siku ya Jumanne zilianza kubeba wajibu wa wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Nchi tano -- Ecuador, Japan, Malta, Msumbiji na Uswisi -- siku ya Jumanne zilianza kuchukua majukumu ya kuwa wanachama wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Muda wao wa miaka miwili ulianza rasmi Januari 1, lakini siku ya kwanza ya kazi ya Baraza la Usalama kwa Mwaka 2023 baada ya likizo ya Mwaka Mpya ni Jumanne, Januari 3.

Hafla ya ufungaji wa bendera za taifa za nchi hizo ilifanyika kuashiria kuanza kubeba wajibu wao. Hafla hiyo ilianzishwa na Kazakhstan Mwaka 2018.

Mwakilishi wa kudumu wa Kazakhstan katika Umoja wa Mataifa Akan Rakhmetullin, ambaye aliongoza hafla hiyo, ameeleza imani yake kwamba nchi wanachama hao watano wapya wa baraza la usalama wataleta mchango wa kina na kuzingatia masuala muhimu ya amani na usalama duniani.

"Tunapoanza mwaka mpya, ni wazi kuwa hali ya Dunia inaendelea kuashiria changamoto na shida nyingi, kutoka kwa migogoro inayoendelea na majanga ya kibinadamu hadi athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi na janga la UVIKO-19," Rakhmetullin amesema.

Amesema ili kushughulikia masuala haya makali kunahitaji ushirikiano na mshikamano pamoja na kujitolea kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Wawakilishi wa kudumu wa nchi tano wajumbe wapya wa baraza walitoa hotuba fupi kabla ya kuweka bendera zao za taifa nje ya ukumbi wa Baraza la Usalama.

Nchi hizo tano zimechukua nafasi ya India, Ireland, Kenya, Mexico na Norway.

Baraza la Usalama lenye wanachama 15 lina wanachama watano wa kudumu -- Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Marekani, na nchi wanachama 10 wasio wa kudumu wanaochaguliwa kwa mihula ya miaka miwili na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wanachama watano wasio wa kudumu kati yao hubadilishwa kila mwaka.

Albania, Brazili, Gabon, Ghana na Umoja wa Falme za Kiarabu ziko katikati ya muhula wao wa miaka miwili kama wanachama wasio wa kudumu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha