99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kamati ya Kodi na Mapato ya Bunge la Marekani yapiga kura kutoa ripoti kuhusu marejesho ya kodi ya Trump (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 22, 2022
Kamati ya Kodi na Mapato ya Bunge la Marekani yapiga kura kutoa ripoti kuhusu marejesho ya kodi ya Trump
Picha hii iliyopigwa Tarehe 20 Desemba 2022 ikionyesha jengo la Bunge la Taifa la Marekani, Capitol huko Washington, D.C., Marekani. Kamati ya Kodi na Mapato ya Bunge la Taifa la Marekani imeipiga kura Jumanne ili kutoa ripoti juu ya marejesho ya malipo ya kodi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Kamati ya Kodi na Mapato ya Baraza la Chini la Bunge la Taifa la Marekani imepiga kura Jumanne ili kutoa ripoti kuhusu marejesho ya malipo ya kodi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump.

Kamati hiyo ya Bunge, ikiongozwa na Wabunge wa Chama cha Democrat, imeidhinisha hatua hiyo kwa misingi ya kichama. Ripoti hiyo itajumuisha maelezo kuhusu marejesho ya malipo ya kodi ya Chama cha Republican kuanzia Mwaka 2015 hadi 2020.

Bado inaendelea kujadiliwa ni lini umma utaona ripoti hiyo. Kamati hiyo imesema itatoa taarifa za kibinafsi kutoka kwenye nyaraka za malipo ya kodi.

Trump alikataa kutoa ripoti zake za malipo ya kodi wakati wa kampeni yake ya urais Mwaka 2016 na miaka minne akiwa katika Ikulu ya White House, na kuvunja mfano mzuri katika siasa za Marekani.

Tangazo la kamati hiyo ya baraza la chini la bunge la Marekani linakuja siku moja baada ya kamati teule ya Baraza la chini la Bunge la Taifa la Marekani inayochunguza ghasia za Capitol za Januari 6, 2021, kumpeleka Trump kwa waendesha mashtaka wa Serikali Kuu kwa ajili ya mashtaka kadhaa ya jinai.

Trump, ambaye amezindua mpango wake wa tatu wa kuingia tena Ikulu ya White House mwezi uliopita, amekosoa mara kwa mara uchunguzi unaohusiana naye, na kuuelezea kuwa wa kisiasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha