Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Australia wafanya mazungumzo ya kimkakati
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong wamefanya Mazungumzo ya sita ya Mambo ya Nje na Kimkakati ya China na Australia hapa Beijing siku ya Jumatano.
Wang Yi ameeleza kuwa ziara ya Wong inafanyika sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na ina umuhimu wa kiishara.
Amesema China na Australia hazina matatizo ya kihistoria wala migongano ya kimsingi ya kimaslahi, na pande hizo mbili zinapaswa na zinaweza kuwa washirika wa ushirikiano unaohitajika.
Wang amesema, kudumisha maendeleo mazuri na tulivu ya ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa China na Australia kunasaidia kikamilifu maslahi ya kimsingi ya watu wa pande zote mbili, na pia kunasaidia kuhimiza amani na maendeleo katika eneo la Asia na Pasifiki na Dunia.
Wang amesema China inashukuru nia ya serikali mpya ya Australia kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza kwa pamoja makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili ili kufikia lengo hilo.
Wang amesema pande zote mbili zinapaswa kuzingatia ahadi zilizotolewa wakati wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, kushikilia maelewano sahihi na njia ya kukomaa ya kutendeana, na kudumisha utulivu wa sera.
Kwa upande wake Wong amesema kanuni za kuheshimiana, kuwa na usawa, kunufaishana na kuishi pamoja kwa amani zilizowekwa na Australia na China wakati wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia zimekuwa na nafasi muhimu katika kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili.
Uhusiano thabiti na ulio wa kiujenzi wa Australia na China hutumikia maslahi ya nchi hizo mbili na kanda. Wong amesema kuwa serikali mpya ya Australia inafuata sera ya kuwepo kwa China moja, inasimamia ipasavyo badala ya kukuza tofauti kati ya nchi hizo mbili, na kurejesha na kuendeleza mawasiliano na mabadilishano katika sekta mbalimbali chini ya mfumo wa ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili kati ya Australia na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma