

Lugha Nyingine
Kamati Teule ya Bunge la Marekani inayochunguza ghasia za Capitol yatoa rejea za uhalifu (4)
WASHINGTON - Kamati Teule ya Bunge la Marekani inayochunguza ghasia za Januari 6, 2021 kwenye Bunge la Marekani, Capitol imetuma rejea za uhalifu kwa Wizara ya Sheria ya Marekani (DOJ) Jumatatu alasiri.
Kamati hiyo imemshutumu Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa kuchochea uasi, njama ya kulaghai Marekani, kula njama ya kutoa taarifa ya uongo, na kuzuia shughuli rasmi.
Marejeleo ya jinai hayalazimiki kisheria, na ni juu ya DOJ kuamua iwapo itafuatilia mashtaka, kwa mujibu wa wachambuzi wa sheria wa Marekani.
DOJ inaendesha uchunguzi wake yenyewe kuhusu ghasia za Capitol, ambapo wafuasi wa Trump walivuruga kikao cha pamoja cha Bunge la Wawakilishi mnamo Januari 6, 2021, ili kuthibitisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa Mwaka 2020.
Mgombea wa Chama cha Republican, Trump alishindwa na Mgombea wa Chama cha Democrat Joe Biden katika kinyang'anyiro cha Ikulu ya White House Mwaka 2020 lakini amekataa kukiri kushindwa na anaendelea kuendeleza madai ambayo hayajathibitishwa kwamba uchaguzi uliibiwa.
Kamati hiyo, inayoundwa na Wabunge saba kutoka Chama cha Democrat na wawili kutoka Chama cha Republican, pia ilipiga kura kuidhinisha ripoti yake ya mwisho katika kikao cha Jumatatu, ambayo itatolewa leo Jumatano kwa saa za Marekani.
Trump, ambaye amezindua mpango wake wa tatu kuitafuta Ikulu ya White House mwezi uliopita, mara kwa mara ameikashifu kamati hiyo na kuelezea uchunguzi na maswali mengine yanayomhusu kuwa yamechochewa kisiasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma