Katibu Mkuu wa UN asema Mkataba wa Sheria ya Bahari ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote (2)
![]() |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kwenye jukwaa na kwenye skrini) akihutubia mkutano wa Baraza Kuu kuadhimisha miaka 40 tangu kupitishwa na kufungua kwa kutiwa saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sheria ya Bahari, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Desemba. 8, 2022. (Eskinder Debebe/Picha ya UN/Kutumwa Xinhua) |
UMOJA WA MATAIFA - Kadri bahari iko "katika hali mbaya," Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari uliopitishwa miaka 40 iliyopita ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Alhamisi.
Guterres ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kuadhimisha miaka 40 tangu kupitishwa na kufungua kwa kutiwa saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sheria ya Bahari, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Mkataba huo uliopitishwa Mwaka 1982, ulifungua sura mpya ya usimamizi wa baharini duniani, na umesaidia sana binadamu kuelewa, kulinda na kutumia bahari.
Miongo minne iliyopita, Dunia ilichukua hatua muhimu kuleta usimamizi na utulivu katika bahari kuu na bahari nyinginezo, Guterres amesema, huku akiongeza kuwa kukubalika kwa mkataba huo karibu na nchi zote kunaonyesha "umuhimu wake wa kimsingi" na mfumo wake wa kisheria na vyombo husika vya nchi kote duniani.
"Tunapokusanyika leo, mkataba huo ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote. Bahari iko katika hali mbaya," mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameonya.
Takriban asilimia 35 ya wavuvi duniani wamenyonywa kupita kiasi, amesema, pia akitoa mfano wa kupanda kwa kina cha bahari, kutia tindikali baharini, kupauka na kufa kwa miamba ya matumbawe, pamoja na "mafuriko makubwa" yanayotishia miji ya pwani na nchi za visiwa vidogo zinazoendelea.
Mpango kabambe unahitajika kwa bahari na watu wanaoitegemea, na maadhimisho haya ya miaka 40 yanaapaswa kuwa "ukumbusho muhimu wa kuendelea kutumia chombo hiki muhimu kukabiliana na changamoto za leo," Guterres amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma