

Lugha Nyingine
Rais wa Tunisia aishukuru China kwa msaada wa muda mrefu kwa maendeleo ya Tunisia (2)
![]() |
Rais wa Tunisia Kais Saied (Kulia) akikutana na Balozi wa China nchini Tunisia Zhang Jianguo mjini Tunis, Tunisia, Desemba 7, 2022. (Ikulu ya Tunisia/Kutumwa Xinhua) |
TUNIS - Rais wa Tunisia Kais Saied Jumatano alipongeza ushirikiano kati ya Tunisia na China, na kutoa shukrani zake kwa msaada wa muda mrefu wa China kwa maendeleo ya Tunisia.
Kwenye mkutano wake na Balozi wa China anayemaliza muda wake nchini Tunisia Zhang Jianguo, Saied alisema urafiki wa Tunisia na China una historia ndefu na unabaki kuwa mpya kila wakati.
“Fursa mpya za maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili zitajitokeza wakati wa kuitishwa kwa Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za China na Kiarabu,” Rais Saied ameongeza.
Amesisitiza kuwa Tunisia iko tayari kushirikiana na China ili kuimarisha urafiki wa pande hizo mbili na kuhimiza uimarishaji wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Pia amemshukuru Zhang kwa mchango wake katika kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili na urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili.
Kwa upande wake, Zhang amesema China na Tunisia zimekuwa zikielewana na kusaidiana katika masuala ya maslahi ya msingi na yanayofuatiliwa na pande zote.
China iko tayari kuungana mkono na Tunisia ili kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili katika ngazi mpya, balozi huyo ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma