99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wapalestina 5 wauawa na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi, huku UN ikitaka kuleta matumaini kwa Wapalestina (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2022
Wapalestina 5 wauawa na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi, huku UN ikitaka kuleta matumaini kwa Wapalestina
Watu wakiomboleza wakati wa mazishi ya Wapalestina waliouawa kwenye mapigano na wanajeshi wa Israel, katika kijiji cha Beit Rima karibu na Mji wa Ramallah, Kando ya Magharibi ya Mto Jordan, Novemba 29, 2022. (Picha na Ayman Nobani/Xinhua)

RAMALLAH/GAZA - Wapalestina watano wameuawa katika mapigano na wanajeshi wa Israel katika matukio manne tofauti katika Kando ya Magharibi ya Mto Jordan, na kusababisha kulaaniwa na kutoa wito wa kusitishwa kwa ghasia za Israel dhidi ya Wapalestina.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Korosi Jumanne amesisitiza umuhimu wa kuleta matumaini kwa Wapalestina, hasa kizazi cha vijana.

"Tunajua kutokana na uzoefu kwamba hakuna kitu kinachochochea hali isiyo na usalama na ghasia zaidi ya giza na kukata tamaa. Lazima tutafute njia ya kurejesha matumaini miongoni mwa Wapalestina, hasa kizazi cha vijana," Korosi ameuambia mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, ambayo huadhimishwa Novemba 29 kila mwaka.

 

Mapema siku ya Jumanne, Wizara ya Afya ya Palestina ilisema katika taarifa yake kwamba ndugu wawili wa Palestina Jawad Al-Rimawi mwenye umri wa miaka 21, na Zafer Al-Rimawi mwenye umri wa miaka, 22, waliuawa baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel karibu na kijiji cha Kafr Ein karibu na Mji wa Ramallah, Kaskazini Magharibi mwa Kando ya Magharibi ya Mto Jordan.

Wizara hiyo imesema katika taarifa tofauti kwamba Mpalestina wa tatu, aliyetambulika kwa jina la Mufid Ikhalyel, aliuawa wakati wa mapigano na wanajeshi wa Israel katika kijiji cha Beit Ummar Kaskazini mwa mji wa Hebron ulioko Kusini mwa Kando ya Magharibi ya Mto Jordan.

Mpalestina wa nne aliuawa baada ya kupigwa risasi kifuani na wanajeshi wa Israel wakati wa mapigano yaliyozuka katika kijiji cha Al-Mughayyar karibu na Ramallah.

Al-Mughayyar Amin Abu Alia, mkuu wa baraza la kijiji, amesema kuwa kwenye mapigano kati ya vijana wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel katika kijiji hicho, mwanamume wa Kipalestina aliyefahamika kwa jina Raed al-Naasan, 21, aliuawa.

Mauaji ya Al-Naasan yamefanya jumla ya Wapalestina waliouawa na Israel tangu Januari kufikia 206, wakiwemo 50 katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa takwimu rasmi.

Hakujatolewa kauli ya mara moja ya Israeli juu ya matukio katika Ukingo wa Magharibi. Hata hivyo, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel katika taarifa yake, Mpalestina wa tano aliuawa baada ya kufanya shambulio Mashariki mwa Ramallah.

Siku ya Jumanne, Palestina ililaani mauaji ya Israel ya Wapalestina hao

Mauaji ya Wapalestina hao watano yanakuja huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya Waisraeli na Wapalestina tangu Machi 2020. Jeshi la Israel hufanya uvamizi wa kila siku katika kando ya Magharibi ya Mto Jordan kujibu mashambulizi yanayofanywa na Wapalestina. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha