99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Reli ya China-Thailand yaleta matumaini ya Thailand kwa urahisi na ustawi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2022
Reli ya China-Thailand yaleta matumaini ya Thailand kwa urahisi na ustawi
Picha iliyopigwa Septemba 7, 2022 ikionyesha eneo la ujenzi wa reli ya China-Thailand katika Jimbo la Nakhon Ratchasima, Thailand. (Xinhua/Lin Hao)

BANGKOK - Akikumbuka utoto wake, Pannaros Boonserm anasema reli iliunganisha nyumbani kwake huko Chiang Mai na sehemu wanakoishi babu na bibi yake katika Jimbo la Nakhon Ratchasima, Kaskazini Mashariki mwa Thailand.

"Mimi na wazazi wangu tulilazimika kutumia muda mwingi kwenye treni," anasema mtafsiri huyo mwenye umri wa miaka 32 katika mradi wa ujenzi wa reli ya China-Thailand, huku akibainisha kwamba kutazama nje ya dirisha kwenye mandhari na miji inayopita polepole imekuwa jambo la kustaajabisha la kumbukumbu ya utotoni isiyoisha.

Treni nchini Thailand zinachosha watu katika safari ndefu kwa sababu zinaenda polepole sana, anasema, huku akieleza matumaini yake kwamba reli ya kasi ya China-Thailand itakamilika na kuanza kazi haraka iwezekanavyo.

"Babu na nyanya yangu wamefikisha miaka yao ya 80. Wanataka kutembelea marafiki zao huko Bangkok, lakini wana wasiwasi kuhusu kusafiri kwa muda mrefu. Ndiyo maana wanafurahi sana kujua kwamba reli inajengwa," Pannaros anasema.

Reli ya China-Thailand, ambayo ni sehemu muhimu ya mtandao wa reli ya kati ya Asia, itakuwa reli ya kwanza ya kiwango cha standard gauge ya mwendokasi nchini Thailand. Sehemu ya kwanza, inayounganisha mji mkuu wa Thailand wa Bangkok na Jimbo la Nakhon Ratchasima, inatarajiwa kufupisha muda wa kusafiri kutoka zaidi ya saa nne hadi zaidi ya saa moja.

"Inatuletea matumaini," anasema. Boonserm anaamini kuwa reli hiyo siyo tu itarahisisha safari za wakazi wa eneo hilo, lakini pia itasaidia kufufua sekta ya utalii na ukuaji wa uchumi katika majimbo yaliyo njiani.

Ikikamilika, reli ya China-Thailand itatumia treni kutoka Bangkok hadi mji wa mpaka wa Nong Khai, ambapo daraja litaiunganisha na reli ya China-Laos. Kufikia wakati huo watu wataweza kusafiri kwa treni kutoka Bangkok, kupitia Laos, hadi Kunming, nchini China.

Wachambuzi wanasema reli ya China-Thailand, ikishaanza kutumika, siyo tu itaingiza uhai katika maendeleo ya kiuchumi ya maeneo yaliyo kando ya njia hiyo nchini Thailand, lakini pia itaimarisha mtandao wa reli ya kati ya Asia na kuhimiza mawasiliano ya kikanda.

Kwa Viroj Lubkritcom, mhandisi wa Thailand mwenye umri wa miaka 59, reli ya China-Thailand ni zaidi ya miundombinu ya muunganisho na itafanya kazi ya kuimarisha uhusiano kati ya watu wa eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha