

Lugha Nyingine
Vyakula vya Kichina vyapendwa na kuwa faida kwa ujuzi wa mpishi wa Namibia (3)
![]() |
Mpishi wa Namibia akionyesha chakula cha Kichina kwenye mkahawa huko Windhoek, Namibia, Novemba 12, 2022. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua) |
WINDHOEK - Tangu kuhamia Windhoek, mji mkuu wa Namibia, mwanzoni mwa miaka ya 1990, Tuhafeni Sem amefanya kazi nyingi za kawaida katika maeneo mengi, lakini ilikuwa ni kwenye Mkahawa wa Kichina Mwaka 1997 wakati ukakamavu na upendo wa vyakula vya Kichina ulimchochea katika kuinua ujuzi wa mapishi.
Sem anafanya kazi kama Mpishi wa Chez Wou, ambao ni mgahawa wa Kichina kutoka Country Club huko Windhoek. Chez Wou ni jina la mkahawa unaotoa ladha halisi za vyakula vya Kichina kwa maelfu ya wenyeji kila mwaka.
"Nilipojiunga, haikunichukua muda mrefu kujifunza, na niliendelea kuwa mpishi baada ya mwaka mmoja," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Huku kukiwa na shauku inayoongezeka ya vyakula vya Kichina, Sem anaongoza kwa mtindo unaokua wa wenyeji kupika vyakula vya Kichina.
"Lengo langu ni kushiriki China kidogo na watu wa Namibia. Chakula hakina kikomo, na ninafurahia sana kukipika kwa sababu ni tofauti na chakula changu cha jadi. Hii imenipa mtazamo mpya," amesema Sem, mzaliwa wa Edudja, Mkoa wa Ohangwena, Kaskazini mwa Namibia.
Anahusisha ujuzi wake wa kupika vyakula vya Kichina na mafunzo ya kazini.
"Mafunzo yaliyotolewa na wapishi wa Kichina kwenye mgahawa yalichukua jukumu muhimu katika kutoa uzoefu wa vitendo," Sem mwenye umri wa miaka 48 amesema.
Kwa maoni yake, vyakula vya Kichina vinapendwa na watu wengi nchini Namibia, na siyo tu kwa jamii ya Wachina. Vyakula vya Kichina anavyovipenda zaidi ni pamoja na tambi maarufu, nyama ya ng'ombe, nguruwe, na maandazi.
Mbali na upishi, pia alipata ujuzi wa kutumia mashine za jiko la viwandani.
"Pia nilijifunza kutoka kwa watu wa China maadili ya kazi ya kufanya kazi kwa bidii na kujitolea, jambo ambalo linatia moyo," amesema na kuongeza kuwa pia amepata ujuzi wa kimsingi wa lugha ya Kichina, ambao unawezesha mawasiliano rahisi na wenzake na wateja.
"La muhimu zaidi, kuwa na kazi huongeza thamani kwa maisha yangu katika suala la mipango ya kusaidia familia yangu," amebainisha.
William Cui, meneja wa Mkahawa wa Chez Wou, amesema kuwa kujenga uwezo wa wenyeji na kuajiriwa kunaleta juhudi za kimkakati za mgahawa huo katika kuendeleza ushirikiano.
Mgahawa huo ambao umekuwa ukifanya kazi kwa zaidi ya miaka 10, umeajiri zaidi ya wenyeji watano na wapishi wawili wa Kichina. "Timu inaendesha dhamira yetu ya kukuza upendo kwa vyakula vya Kichina nchini Namibia," William amehitimisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma