

Lugha Nyingine
Phryges watambulishwa kuwa maskoti rasmi wa Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki ya Paris 2024 (6)
![]() |
Picha iliyopigwa Novemba 14, 2022 ikiwaonyesha Phryges, wakizinduliwa kuwa maskoti rasmi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto kwa Walemavu ya Paris 2024 kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Saint Denis, Ufaransa. (Xinhua/Gao Jing) |
PARIS - Waandaaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto kwa Walemavu ya Paris 2024 Jumatatu wamezindua kofia za Phryges kuwa maskoti rasmi wa michezo hiyo.
Maskoti hao wamezinduliwa zikiwa zimesalia zaidi ya siku 600 kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Mwaka 2024. Michezo yote miwili ya Olimpiki na ile ya walemavu, Paralimpiki itatumia muundo sawa wa maskoti wenye tofauti kidogo.
"Maskoti daima wamechukua nafasi maalum katika historia ya Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki," Rais wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 Tony Estanguet amesema. "Wanatengeneza mshikamano wa kihisia kati ya Michezo na watu, na kuchangia hali na moyo wa tamasha katika viwanja vya michezo na maeneo mengine ya Olimpiki."
Bidhaa zilizoidhinishwa za maskoti hao zitapatikana kuanzia Novemba 15 kwenye duka rasmi la Paris 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma